Saturday, December 24, 2011

Historia ya Kiswahili

Historia ya Kiswahili
Historia ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.

Neno Swahili ni neno la asili ya Kiarabu Sahil lenye maana ya pwani; sawahil ’’as-sawāhilī’’ (السواحلي) ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni wa eneo la pwani.

Mwanzo katika miji ya pwani

Kiswahili kilianza kama lugha ya miji na mabandari ya biashara ya kimataifa kwenye pwani la Afrika ya mashariki. Tuna historia jinsi gani miji kama vile Kilwa, Lamu na mingine kadhaa ilianzishwa na wafanyabiashara Waarabu au Wajemi waliooa wenyeji. Idadi ya wahamiaji kutoka Uarabuni haikuwa kubwa sana hivyo lugha ya wenyeji ilitumika kila mahali ila tu maneno mengi yameingia kutoka Kiarabu. Kwa ujumla Kiswahili ina maneno ya asili ya Kiarabu kati ya 30-40%, hali inayolingana na kiasi cha maneno ya asili ya Kilatini au Kifaransa katika lugha ya Kiingereza. Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu. Hivyo Kiswahili kilizaliwa kuwa lugha ya Kibantu kilichopokea maneno mengi ya asili ya nje. From http://sw.wikipedia.org/wiki/Historia_ya_Kiswahili
Read more »